EXCLUSIVE : NI WAKATI WAKO SASA KUTIMIZA NDOTO YAKO WEWE KIJANA MWENYE KIPAJI CHOCHOTE.


Hapa ndo wanapopaita Escape One iliyopo Mikocheni, mbele kidogo na Clouds mkono wa kulia kama unaelekea Kawe. Humu ndo kutafanyika utafutaji wa vipaji vya aina tofauti kila siku ikiongozwa na Team nzima ya Step Up Player kutoka Clouds Tv, Higher Learning na Uni-Kitaa na
dhumuni kuu ni kusaidia vipaji vichanga kufikia malengo yao. Shiriki sasa kwa shillingi Elfu kumi tu, upate fursa ya kufanya free video production itayorushwa kwenye kipindi cha Step Up Player kinachorushwa Clouds Tv kila Jumatatu hadi Ijumaa saa sa12 nanusu jioni hadi sa1 jioni, free photo shoots, free counseling kutoka kwa timu yetu na staa aliyealikwa kisha kupata mda wakuenjoy nawenzako huku mkishushia mshkaki na soda, vyote bure kwa Elfu kumi tu.
Usisahau ukionyesha kipaji chako vizuri utambulia zawadi na hela kila weekend, kuwepo chini ya reality house itayofanyika muundo kama wa "Big Brother' baada ya mwezi mmoja nanusu. Unasubiri nini? Tukutane Escape One.
For more details visit @universitycorner in IG